IQNA

Msikiti wa Bristol, Uingereza  kuandaa Futari kubwa

20:55 - March 24, 2025
Habari ID: 3480428
IQNA – Kama miaka iliyopita, tukio la Futari Kubwa litafanyika katika mji wa Bristol, Uingereza, mwaka huu. 

Futari hiyo inayopendwa sana itafanyika katika makao yake ya awali kwenye Barabara ya St Mark's baadaye. Mwaka huu, kutokana na mahitaji makubwa na hali ya hewa isiyotabirika, tukio hilo litafanyika ndani ya Msikiti wa Easton Jamia saa 18:00 GMT.

Watu kutoka dini na jamii tofauti wanakaribishwa kujiunga na Futari, ambayo ni chakula ambacho Waislamu hula wakati wa Magharibi au jua kuzama katika mwezi mtakatifu wa Ramadhani. Abdul Malik, mwenyekiti wa Msikiti wa Easton Jamia, alisema kuwa kuwa na tukio hilo ndani kutawawezesha watu kujionea "uzuri" wa msikiti huo.

"Tuna misikiti mizuri katika jiji hili," alisema Malik. "Nafikiri ni fursa nzuri kuwaleta watu kwenye msikiti ili waone uzuri wa ndani ya msikiti, lakini pia kwa watu kujifunza kuhusu Uislamu."

Futari Kubwa ilizinduliwa kwenye Barabara ya St Mark's mwaka 2017 na tangu wakati huo imekuwa tukio muhimu katika mji wa Bristol. Mwaka huu, kutokana na mahitaji makubwa na hali ya hewa isiyotabirika, itafanyika ndani ya msikiti.

Wageni watafungua saumu zao pamoja kwa njia ya kitamaduni kwa kutumia tende na maji. Chakula kilichopakiwa kitatolewa, na ikiwa hali ya hewa itaruhusu, wageni wataweza kuendelea na chakula chao cha Futari katika mazingira ya pamoja nje ya msikiti

Kutokana na kiwango cha juu cha wanaotaka kuhudhuria, tukio la mwaka huu limetengwa kwa watu 500 tu na tiketi zote zimeshasambazwa. Ili kuhakikisha kuwa Futari Kubwa inakuwa na uendelevu, waandaaji wanatazamia mipango ya kubuni hema ikubwa itakayowezzesha tukio hilo kufanyika katika hali yoyote ya hewa.

3492478

captcha